#Glm News | Kiss Daniel kupamba uzinduzi wa tamasha la ‘Monte Carlo Classic’ Dar

wpid-wp-1452943456596

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki, ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Monte Carlo Classic tukio lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.

pamoja

Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa tukio hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.

Akizungumza mapema leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya tukio hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.

Aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000. Alisema tukio la the Monte Carlo Classic limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burudani.

Danile

Kiss Daniel akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dar Ijumaa hii

Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.

Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii benki hiyo. Tunayofuraha kuwa sehemu ya uzinduzi wa tukio hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.

meneja

Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, akiongea na waandishi wa habari

“Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. Mwezi uliopita Benki ya Bacrays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania. Kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tunapenda kuwahamasisha kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili,” alisema

Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.

“Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”

Msanii huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye tukio hili.
Msanii huyo alizaliwa Mei Mosi, 1994 katika mji wa State, Kiss Daniel ni mwimbaji maarufu anayetamba na kibao chake cha Woju alichokiachia mwaka 2015 a kutamba kwenye vituo mbalimbali vya runinga na redio akimshirikisha Davido na Tiwa Savage.

2016-08-26

Kwa hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa Jombo.
Mwisho